Timu ya Signal imejitolea kwa dhamira ya kutengeneza teknolojia huria ya faragha ambayo inalinda uhuru wa kujieleza na kuwezesha mawasiliano salama ya kimataifa. Mchango wako unachochea dhamira hii. Hakuna matangazo. Hakuna wafuatilizi. Hakuna mzaha.

Mchango wako unasaidia kufadhili utengenezwaji, seva na mkongo wa mawasiliano wa programu inayotumika na mamilioni ya watu kote duniani kwa ajili ya mawasiliano ya faragha na ya haraka.

Kama ukitoa barua pepe, utapata uthibitisho wa barua pepe kwa ajili ya kumbukumbu za kodi. Signal Technology Foundation ni shirika linalojitegemea lisilo la faida na lisilotozwa kodi chini ya kifungu cha 501c3 cha Kanuni ya Mapato ya Ndani. Nambari yetu ya Kitambulisho cha Ushuru ni 82-4506840.

Kumbuka: Signal haiwezi kutoa beji kama ukichangia hapa tofauti na kutumia Google Pay au Apple Pay ndani ya programu ya Signal.


Changia sarafu ya crypto

Michango ya sarafu ya crypto kwa Signal inachakatwa kupitia The Giving Block.

Kama unataka kupata punguzo la kodi Umarekani kwa ajili ya bei shindani ya soko ya mchango wako wa sarafu ya crypto, unaweza kutoa barua pepe yako kwa hiari ili kupata risiti ya kodi. The Giving Block pia inapokea michango ya siri.