Ongea kwa Uhuru

Sema "habari" kwa uzoefu tofauti wa kutuma jumbe. Uzingatiaji usiotarajiwa kwenye faragha, ukiunganishwa na vipengele vyote unavyotarajiwa.


Pata Signal

Kwanini utumie Signal?

Chunguza hapa chini kuona kwa nini Signal ni programu ya kutuma jumbe iliyo rahisi, yenye nguvu, na salama

Shirikisha Bila Hofu ya Ukosefu wa Usalama

Msimbo fiche (unaowekwa na Itifaki ya Signal ya chanzo huria) huweka mazungumzo yako salama. Hatuwezi kusoma jumbe zako au kusikiliza simu zako, na hakuna mtu mwingine anayeweza. Usiri sio njia ya hiari — bali namna ambavyo Signal hufanya kazi. Kwa kila ujumbe, kila simu, kila wakati.

Sema Chochote

Shirikisha jumbe, jumbe za sauti, picha, video, GIFs na mafaili bure. Signal inatumia muunganisho wa data ya simu yako ili uweze kuepuka ada za jumbe za SMS na MMS.

Ongea kwa Uhuru

Piga simu za kawaida na za video kwa sauti inayosikika vyema kwa watu ambao wanaishi mjini au wanaishi nje ya nchi, bila malipo ya kimataifa.

Tengeneza Vibandiko vya Faragha

Ongeza safu mpya ya kujieleza kwenye mazungumzo yako kwa vibandiko vilivyosimbwa. Unaweza pia kutengeneza na ku-share pakiti za vibandiko vyako.

Kutana na Vikundi

Gumzo za vikundi hufanya iwe rahisi kuendelea kuwasiliana na familia yako, marafiki, na wafanya kazi wenzako.

Hakuna matangazo. Hakuna wafuatiliaji. Hakuna mzaha.

Hakuna matangazo, hakuna wauzaji wa ushirika, na hakuna ufuatiliaji wa kuogofya kwenye Signal. Kwa hivyo zingatia ku-share nyakati muhimu na watu unaowajali.

Bure kwa Kila Mtu

Signal ni shirika huru lisilo la faida. Hatuhusishwi na kampuni yoyote kubwa ya teknolojia, na kamwe hatuwahi kununuliwa na yoyote aidha. Maendeleo yanawezeshwa na ruzuku na michango kutoka kwa watu kama wewe.

Changia Signal